Home » » ZIJUWE HAKI NA WAJIBU WA MTEJA WA BIMA

ZIJUWE HAKI NA WAJIBU WA MTEJA WA BIMA


HAKI NA WAJIBU WA MTEJA WA BIMA

Wasomaji wa makala hii, ni matumaini yangu muwazima na wenye afya tele kama mwenyezi mungu alivyo wajalia.
Leo tutaangalia haki na wajibu wa mteja wa bima lakini kabla ya kuendelea mbele, ni muhimu kutambua maana ya Bima.

Bima inatafsiliwa kama uhamishwaji riski za kiuchumi kutoka kwa mkataji wa Bima kwenda kwa mtoaji wa Bima zinaweza leta hasara za kifedha kutokana na matukio yasiyo tarajiwa ambayo huathiri mali, maisha au mwili kwa kuzingatia vigezo ambavyo hutolewa na mtoaji Bima. Zifuatazo ni haki na wajibu wa mkataji wa bima;
 
 Ni haki ya mkataji wa Bima kufidiwa katika hasara ya mali ambayo imeharibiwa kulingana na ukaribu wa mazingira yaliyo ainishwa katika sera za Bima (nearest cause/causa proxima) ambapo mtoaji Bima huangalia chanzo cha ajali na athari katika mali ilikujua kuw ani kweli mali imeharibika kulingana na mazingira au ukaribu wa mazingira yaliyo kwenye sera z a Bima hiyo.

 Ni haki ya mkataji wa Bima kufidiwa kwa hasara aliyoipata ili aweze kunufaika na mali yake kama ilivyo kuwa mwanzo pindi mali yake haijaharibiwa. Fidia hiyo ni lazima isipungue na isizidi gharama ya mali husika, kwani bima haipo kwa ajili ya kumtajirisha ama kumzorotesha mkataji Bima kiuchumi, bali kumrejesha katika sehemu aliyokuwepo kabla hajakumbwa na matatizo. Fidia hiyo huwa katika mfumo wa kifedha, ama utengenezaji wa mali iliyo haribika au kupatiwa mali nyingine.

 Riba ya Bima ni haki ya makataji wa Bima ambayo huundwa kimkataba na sheria zingine ikiwemo na sheria ya uwingereza (common law)
 
Ni wajibu wa mkataji wa Bima kutoa ukweli na ushirikiano wa hali ya juu(utmost good faith) wa taarifa zinazo husiana na mali husika iliyo katiwa Bima, kwa mfano kama ni Gari, basi ueleze lina muda gani tangu linunuliwe hua unali hifadhi wapi, eneo eleza mazingira hatarishi ya sehemu unapo lipaki ili mtoaji Bima aweze tambua anakukatia Bima ya kiwango gani. Ama kama anaweza kukubali au kukatalia kulingana na mazingira ya mali yako. Mfano mwingine ni wa nyumba ambayo ipo kalibu na ghara la kuhifadhia vitu vinavyo lipuka. Hivyo vyote ni wajibu wa mkataji Bima kuvitaja kwa mtoa Bima hata kama hajaulizwa. Wajibu wa kutoa ukweli wa hali ya juu hubaki katika kipindi chote cha makubaliano kabla ya kuingia katika mkataba mpaka mkataba unapokamilika ndipo wajibu huu hubadilika na kuwa ukweli wa kawaida juu ya mali husika (simple good faith)
 
Ni wajibu wa mkataji Bima kujitahidi kupunguza hasara ama kwa kujitahidi kuepusha majanga yasiyo tarajiwa kadri awezavyo ili kulinda mali yake kama vile katika mlipuko wa moto ni vema mkataji Bima akapambana na moto kadri awezavyo ili kunusuru mali yake sio kupuuza kwa mantiki kwamba mali hiyo ameikatia Bima.

 Ni wajibu wa mkata Bima kulipa kiwango cha fedha alicho pungukiwa na mtoa Bima, ambapo pia ni wajibu wa mtoa Bima kumpatia mkataji Bima sera za Bima ambazo anatakiwa akubaliane nazo.

 Ndugu msomaji wa makala hii, hivyo ndivyo vitu vya msingi unavyopaswa vitambua kama haki na wajibu wa mkataji wa bima.

IMEANDALIWA NA CUTHBERT BANDIHO.


Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BC LEGAL INFORMER - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger