FAHAMU JINSI YA KUJENGA KESI YAKO KWA KUBOMOA USHAHIDI WA UPANDE WA PILI MAHAKAMANI

Makala hii inahusu watu wanaopeleka kesi zao mahakama ya mwanzo.
 Kwa Tanzania mahakama hii ndio mahakama isiyo ruhusu mawakili wasomi kuwakilisha wateja wao katika kesi mbali mbali ambazo zipo chini ya mamlaka ya mahakama hii.

Kutokana na hofu ya kuingia mahakamani, au kuhukumiwa watu wengi hushindwa kujitetea ipasavyo na mwisho kupoteza haki zao, hivyo basi hapa utajifunza jinsi ya kujenga kesi yako kwa kubomoa ushahidi wa upande wa pili.

Pindi unapopewa nafasi ya kumuuliza maswali shahidi, jaribu kwenda kwa mtiririko ufuatao.

Muulize shahidi maswali kama yeye anakufahamu, mahali unapoishi, wewe nay eye mlianzaje kufahamiana, shughuli zako unazo fanya, muulize kama anaufahamu mgogoro au kesi hiyo vilivyo, muulize pia kwanini yeye anasimama pale

Endapo unahisi shahidi huyu anatoa ushahidi kwa sababu ulishawahi kukosana nae hapo awali basi ijenge kesi yako kwa kumbana na maswali yanayo onyesha kuwa yupo hapo kwa sababu anakinyongo na wewe.

HUPASWI kuanza kumuuliza maswali yanayo husiana na siku ya tukio moja kwa moja, kwani unaweza kupoteza kesi yako hasa kama ni kesi ya kutengeneza yani watu wamepanga  waje wajenge mazingira ya wewe kufanya kosa hilo.

HIVYO mbane kadri uwezavyo kwa maswali kwa kujenga historia yake na wewe hapo awali kabla ya siku ya tukio au mgogoro. Ili kuweza kumsaidia mheshimiwa Hakimu kuwa Yule shahidi mmefahamianaje na kwa nini yeye ameingia kama shahidi dhidi yako


Unapopewa nafasi ya kuuliza maswali usimwambie hakimu kuwa “huyu ni muongo, siku hiyo mimi sikuwepo….” Mheshimiwa Hakimu hatokusikiliza kwani yeye amekupa nafasi ya kuhoji maswali na sio kujitetea.

Hivyo bomoa ushahidi na ijenge kesi yako kwa kumuhoji maswali shahidi tangu kabla mgogoro haujatokea mpaka ulipotokea ili hakimu aweze fahamu historia yenu na mpaka kupelekea mgogoro hapo Mheshimiwa hakimu atakukwa amepata story kamili kupitia maswali yako


TAMBUA kipengele hiki kimeongelea pindi mlalamikaji au mlalamikiwa anapopewa nafasi ya kubomoa ushahidi wa shahidi ni baada ya shahidi kutoa ushahidi wake wa awali kwa lugha ya kisheria tunaita CROSS EXAMINATION.

Vile vile ni vema kutembelea ofisi za mawakili kwa ajili ya ushahuri kabla ya kesi yako kusikilizwa. KUMBUKA Wakili Msomi hana majibu ya kesi yako ila pindi utakapo msimulia, atakuelekeza jinsi ya kuendesha kesi yako na si kukufundusha uongo.

Niimani yangu umejifunza japo kwa ufupi juu ya kubomoa ushahidi wa upande wa pili na hivyo ndivyo unavyoijenga kesi yako mbele ya Mahakama Tukufu.

Imeandaliwa na Mwanasheria Cuthbert

Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

12 comments:

Unknown said...

Ninaomba msaada wa jinsi ya kufuta kesi ya jinai (wizi) mahakama ya mwanzo.

Habari mpya said...

Asante sana

Unknown said...

Unanzidi kunivutia kwenye hii fani. Asante kwa kutupa maarifa

Unknown said...

Naomba kuuliza swali
Kesi ya jinai inachukua mda gani kwa mwanasheria kuifikiaha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika

Unknown said...

Naweza nikapate contact zako, Nina shda ,nataka kuelekezwa

Unknown said...

HV ,kama ninamtu na kesi wilaya tofauti na police waliohusika ni wilaya tofauti na ya kwangu naweza kuchukua hatua gan ili kuhamisha kesi

Unknown said...

Kesi yangu iko polisi ,wilaya tofauti na ya kwangu mim,je naweza kufanyq nini ili nihamishe kesi yangu kwenda kituo cha police kwenye wilaya yangu?

Unknown said...

Mpaka apo nmejifunza

Unknown said...

Asante kwa ufafanuzi mzuri naweza kuongea na wewe kupitia namba gani kwa ajili ya usaidizi wa kisheria.asante

Unknown said...

asant

King said...

Naomba nipate mawasiliano na wewe

Unknown said...

Ningependa kujua jinsi ya kujitetea katika kesi ya mauaji ukisha patikana na shitaka la kujibu

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BC LEGAL INFORMER - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger