Kumekua na dhana ya baadhi ya watu
kuogopa Mahakama, hata pindi wanapoombwa kwenda kutoa ushahidi wa matukio walio
shuhudia wao hukataa.
Sheria
ya mwenendo wa madai [1] imetoa
mwongozo wa kumlazimisha shahidi huyo kuja mahakamani kutoa ushahidi katika
kesi yako.
Hivyo basi kupitia sheria hiyo
utatakiwa kuiomba Mahakama kutoa
wito wa shahidi kuhudhuria Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wowote ule
unaotakiwa kutolewa kwa ajili ya kujenga kesi yako. Hivyo Mahakama itatoa wito
wa shahidi kuhudhuria Mahakamani ( wengi
huifahamu kwa jina samansi)
Endapo shahidi atakataa wito wa
Mahakama, yani atagoma kuja mahakamani katika tarehe tajwa, Mahakama itatoa tangazo ambalo litabandikwa katika
mlango wa nyumba anayoishi au sehemu yoyote ambapo mtu huyu anaweza kuliona
tangazo hilo.
Mahakama pia inaweza kutoa amri ya
kushikiliwa kwa mali ya shahidi huyo na dalali
wa mahakama mpaka atakapo mlipa dalali wa mahakama pamoja na fine au mali
zake kuuzwa vile Mahakama itakavyoona inafaa.
Njia nyingine ni kwamba Mahakama
imepewa mamlaka yakutoa hati ya
kukamatwa kwa shahidi huyo kwa dhamana au bila hata ya dhamana.
Hivyo basi unapaswa kutambua kuwa,
pindi unapohitajika kwenda kutoa ushahidi Mahakamani, unapaswa kuitikia wito
huo ili kuepukana na usumbufu kama ulivyo ainishwa katika sheria ya mwenendo wa madai
TRINITY COAST ATTORNEYS,
POBOX 79490,
DAR ES SALAAM,
5TH FLOOR DARWORTH (BAVARIA) HOUSE,
OFF NYERERE RD., KAMATA TRAFFIC LIGHTS
OPP. NAKUMAT SUPER MARKET
0 comments:
Post a Comment