Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati ganianakusimamisha uwapo barabarani.
Mamlaka ya kusimamisha
gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako kamaatakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani pia anaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako kamaatakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani pia anaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).
Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari anaweza kukataa fotokopi hata hivyo, unaweza kuamua kupeleka leseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa.Ili kuepukamatatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).
Hati ya usajili:
Ofisa wa polisi ana haki
ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili
gari lazima liendane na maelezo yakwenye kibandiko, lakini vitu vidogokama
rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).
Leseni ya barabarani, na bima ya gari:
Ofisa wa polisi ana haki
ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani nakibandiko cha bima
kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).
Kunyang’anywa:
Ofisa wa polisi HANA
haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.
Mikanda ya kiti ya usalama:
Wewe na abiria wako wa
kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari
iwe inatembea au imesimama) unatendakosa kama unaendesha wakati abiria wako
hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria
wote wafunge mikanda.
Kuendesha baada ya kunywa pombe:
Kama ofisa wa polisi
anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka
upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi cha pombe
kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na
hatiaya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).
Kutumia simu ya mkononi
wakatiunaendesha:
ingawa sheria haikatazi
hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la
kuendesha kwa uzembe
(RTA, s.42, s. 50).
Mwendo kasi:
Unapaswa kuzingatia
kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya
hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) ofisa wa polisi anaweza kupima
mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga ushahidi
wake mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).
Kustahili kuwepo barabarani:
Ofisa WA polisi ana haki
ya kukagua Kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki,
taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri unawezakutakiwa
kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi
(RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka.
Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka
polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.
KAMA OFISA WA POLISI
ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA:
Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa
na kulipa faini ya sh. 20,000 kwaofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili
kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezokwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na
nyote wawili mtatia saini kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu
iliyotiwa saini. Unaweza kwenda Na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo.
Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza
jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIAYOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisianakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishi kwa Ofisa Msimamizi Mkuu ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu usitoe rushwa na usipokee rushwa.
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIAYOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisianakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishi kwa Ofisa Msimamizi Mkuu ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu usitoe rushwa na usipokee rushwa.
SOURCE JAMII FORUM.
SHERIA ILIYOTUMIKA INAITWA THE ROAD TRAFIC ACT SURA YA 168.
0 comments:
Post a Comment