NAMNA
YA KUDAI MALIPO YA BIMA
Mdai wa Bima lazima
awe miongoni wa wanufaikaji wa Bima hiyo. Ni lazima awe analipa malipo maalumu
(premium) kama Bima ilivyo elekezwa. Vilevile ni lazima awe amepata hasara kama
ilivyo ainishwa katika sera za Bima hiyo ambayo alikubaliana nazo.
Mdai wa bima
ataandika maombi na kuyapeleka katika kampuni ya Bima. Kampuni itayapokea
maombi yale na kufanya tathmini, hii inajumuisha uchunguzi juu ya tukio lililo
sababisha hasara ambapo hata mahojiano kwa wahusika kufanyika ili kujua na
kujilidhisha kuwa ni kweli ilikua ajali ambayo haikuweza kukingika.
Baada ya hapo
maombi yatapitishwa na mdai wa Bima kufidiwa malipo ya Tax yanaweza kujumuishwa
au mdai kulipia mwenyewe.
Kwa vile Mkataba
wa Bima basi haupo kwa ajili ya kumtajirisha mdai wa Bima basi fidia ni lazima
iwe, kiasi cha fedha kinacho lingana na thamani ya hasara/mali iliyo haribiwa
mali inaweza rekebishwa (repair) au anaweza pewa mali nyingine kwa maana ya
kwamba kurudishwa katika hali ya awali (Reistatement)
Imeandaliwa na Cuthbert Bandiho.
0 comments:
Post a Comment