- Raia ana haki ya kumwomba askari
ajitambulishe kwako.
- Mwulize jina lake
- Mwulize namba yake ya uaskari
- Raia ana haki ya kujulishwa kwanini
anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
- Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu,
jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama
Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia ana haki ya kuomba na kupewa
dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
- Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo
kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo
utakayoandika.
- Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama
Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama
ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
- Raia ana haki ya kuomba Wakili wake
awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo
yake.
- Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya
kutia sahihi yake.
- Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha
ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama
Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
- Raia kama ni mwanamke ana haki ya
kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi
mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
- Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani
katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha
polisi.
Home »
LAW INFORMATION
» TAMBUA HAKI ZAKO PINDI UNAPOWEKWA KIZUIZINI NA POLISI.
TAMBUA HAKI ZAKO PINDI UNAPOWEKWA KIZUIZINI NA POLISI.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan
klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website
Labels:
LAW INFORMATION
0 comments:
Post a Comment