Home » » FAHAMU AINA ZA UMILIKI WA ARDHI

FAHAMU AINA ZA UMILIKI WA ARDHI

SHERIA ZA ARDHI TANZANIA.


 Tunapozungumzia Ardhi kwa mujibu wa sheria ZA Tanzania tunamaanisha ;- Ardhi ni pamoja na  inavyoonekana na vitu vinavyoonekana juu yake, vikiwemo nymba na majengo mengine ya kudumu pamoja na vitu vilivyopo chini ya ardhi isipokuwa madini na mafuta.

Sheria za Ardhi zilitungwa mwaka 1999 na kuanza kutumika rasmi mwaka 2002.
sheria hizi ziko mbili ambazo ni sheria ya Ardhi namba 4 ya 1999 na sheria ya Ardhi ya kijiji namba 5 ya 1999.

Kwa mujibu wa sheria ya Ardhi, umiliki wa ardhi umegawanyika katika sehemu kuu mbili nazo ni
i. Umiliki wa mtu binafsi 
ii. Umiliki wa pamoja

i. umiliki wa mtu binafsi.

sheria inamruhusu mtu yeyote kumiliki ardhi yake binafsi hata kama yupo katika ndoa kwa kufata utaratibu maalumu ambao sheria ya ardhi inaeleza.

ii. Umiliki wa pamoja 
umiliki huu ni umiliki wa ardhi moja zaidi ya mtu mmoja na unafahamika kama co - occupancy nawenyewe umegawanika katika sehemu kuu mbili nazo no ;
a) Umiliki wa pamoja wa hisa au shea zinazogawanyika - tenancy in common.
b) Umiliki wa pamoja wa hisa au shea zisizogawanyika - joint tency


a) Umiliki wa pamoja wa hisa au shea zinazogawanyika - tenancy in common.
Katika umiliki huu ikitokea mmiliki mmoja amefariki hisa/shea yake itahamia kwa warithi wake mfano kaka, dada, mke, mume watoto, nk.

b) Umiliki wa pamoja wa hisa au shea zisizogawanyika - joint tency
Umiliki wa aina hii unatolewa kwa idhini ya mahakama Kuu tu. chini ya umiliki huu, endapo mmiliki mmoja atafariki basi hisa/shea zake zitahamia kwa wamiliki au mmiliki aliyebaki ambayo kwa lugha ya kisheria inaitwa right of survivorship yani haki ya mtu anayesalia. hii inamaanisha kwamba watu wanaotakiwa kumrithi hawana haki bali wale alioshea nao ardhi ndio wenye haki utaratibu huu huenda mpaka kwa mmilik wa mwisho.
Itambulike kuwa ; sheria imeweka bayana kwamba umilik wa pamoja wa hisa/shea zisizogawanyika utakoachukuliwa bila kibali maaalumu kutoka Mahakama Kuu ni ule wa wanandoa na si vinginevyo hivyo ni lazima kwa wengine kupata kibali kutoka Mahakama Kuu.


Mpaka hapo ndugu msomaji wa makala hii umeweza kutambua aina za umiliki wa ardhi hivyo ni muhimu hasa kwa wanandoa kutafakari ni aina gani ya umiliki inawafaa ilikusudi kuepuka migogoro hasa pindi wanapotengani aidha kwa kifo au kwa mujibu wa sheria za ndoa.

written by CUTHBERT BANDIHO Tanzanian Lawyer.
Jika Anda menyukai Artikel di blog ini, Silahkan klik disini untuk berlangganan gratis via email, dengan begitu Anda akan mendapat kiriman artikel setiap ada artikel yang terbit di Creating Website

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BC LEGAL INFORMER - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger