NAFASI ZA AJIRA





JOB VACANCY

Position: SALES AND MARKETING

QUALIFICATIONS   
1.    Degree in Sales and Marketing or equivalent qualification
2.    Age between 20-45
3.    With experience of 1-3years
4.    Certificate of leadership
5.    Must be competent in English and Kiswahili

Come with your updated Cv Application letter and relevant Certificates.

Location ;Mbezi Jogoo, Dar es salaam, Tanzania, Bagamoyo Road,
Contact us through; 0658387041
                                  0658387040

Application letter with attached Cv. should bare the following address or Email
Human Resources and Legal Officer,
Agape Associates limited,
P.O. Box 700029,
Email ; hr@ting.co.tz        
Dar es salaam,
Tanzania.





AJIRA AJIRA AJIRA


JOB VACANCY

Position: TECHNICAL ENGINEER

QUALIFICATIONS   
1.    Degree In media Technology- head end

2.    Age between 25-45

3.    With experience of 1-3years

4.    Certificate of leadership

5.    Must be competent in English and Kiswahili

Come with your updated Cv Application letter and relevant Certificates.

Location ;Mbezi Jogoo, Dar es salaam, Tanzania, Bagamoyo Road,
Contact us through; 0658387041
                                  0658387040

Application letter with attached Cv. should bare the following address or Email
Human Resources and Legal Officer,
Agape Associates limited,
P.O. Box 700029,
Email ; hr@ting.co.tz        
Dar es salaam,
Tanzania.





NAFASI ZA AJIRA




VACANCIES
AGAPE ASSOCIATES LIMITED
Agape Associates Limited immediately invites Applicants with suitable qualifications to fill the following vacant posts.
Position: PRODUCTION MANAGER
DUTIES AND RESPONSIBILITIES
QUALIFICATIONS   
1.      Degree in Journalism or equivalent qualification
2.      Age between 30 - 45
3.      With experience of 1-3years
4.      Certificate of leadership
5.      Must be competent in English and Kiswahili
Come with your updated Cv Application letter and relevant Certificates.
Location ;Mbezi Jogoo, Dar es salaam, Tanzania, Bagamoyo Road,
Contact us through; 0658387041
                                  0658387040
                                              
Application letter with attached Cv. should bare the following address or Email
Human Resources and Legal Officer,
Agape Associates limited,
P.O. Box 700029,
Email ; hr@ting.co.tz        
Dar es salaam,
Tanzania.





Position: BILLING OFFICER
QUALIFICATIONS   
6.      Degree in IT
7.      Age between 18-34
8.      With experience of 1-3years
9.      Certificate of leadership
10. Must be competent in English and Kiswahili
Come with your updated Cv Application letter and relevant Certificates.
Location ;Mbezi Jogoo, Dar es salaam, Tanzania, Bagamoyo Road,
Contact us through; 0658387041
                                  0658387040
                                              
Application letter with attached Cv. should bare the following address or Email
Human Resources and Legal Officer,
Agape Associates limited,
P.O. Box 700029,
Email ; hr@ting.co.tz        
Dar es salaam,
Tanzania.









Position: TECHNICAL ENGINEER
QUALIFICATIONS   
11. Degree in IT
12. Age between 25-45
13. With experience of 1-3years
14. Certificate of leadership
15. Must be competent in English and Kiswahili
Come with your updated Cv Application letter and relevant Certificates.
Location ;Mbezi Jogoo, Dar es salaam, Tanzania, Bagamoyo Road,
Contact us through; 0658387041
                                  0658387040
                                              
Application letter with attached Cv. should bare the following address or Email
Human Resources and Legal Officer,
Agape Associates limited,
P.O. Box 700029,
Email ; hr@ting.co.tz        
Dar es salaam,
Tanzania.











NI VIGEZO GANI MAHAKAMA INAZINGATIA KATIKA KUPUNGUZA ADHABU?




Sheria mbali mbali zinazo zungumzia makosa ya jinai hutaja adhabu ambazo mtu anapaswa kupata kutokana na makosa hayo. Adhabu hizi huweza kuwa faini, kifungo, fidia au vyote kwa pamoja.

Endapo mtuhumiwa atakutwa na hatia ya makosa hayo Mheshimiwa hakimu/Jaji anatakiwa kuzingatia sheria inayotoa adhabu hizo pamoja na sheria ya kima cha chini cha hukumu[1] inaelezaje, bila kusahau baadhi ya kanuni kutoka katika kesi zilizo kwisha amuliwa.

Pindi Mtuhumiwa anapopatikana na hatia Mahakama hutoa nafasi kwa muendesha mashtaka kueleza kwa nini Mtuhumiwa apewe adhabu inayostahili kama sheria inavyotaka na pia mahakama itatoa nafasi kwa mtuhumiwa aliyekutwa na hatia kuiomba Mahakama impunguzie adhabu na kwa sababu zipi.

Kifungu cha sita cha sheria ya kima cha chini cha hukumu kinatoa ruhusa kwa Mahakama kutoa hukumu kwa Mtuhumiwa aliyehukumiwa kwa mara ya kwanza kuhukumiwa kanakwamba sheria hiyo haipo, yani kuhukumu vile itakavyoona inafaa.

Kanuni ambazo mahakama inapaswa kuzingatia katika kutoa hukumu zinainishwa katika kesi ya Jamuhuri dhidi Kidato Abdullah[2] ambazo ni uzito wa kosa hilo, rekodi ya mtuhumiwa, umri, maslahi ya jamii ukilinganisha na maslahi ya mtuhumiwa.

Katika kesi ya Jamuhuri dhidi ya Asia Salum na wengine[3]  Jaji Mnzavas alibadili adhabu ya mama na mwanae ambao walikutwa na hatia ya kumpiga mlalamikaji mpaka kumvunja bega la kushoto na kumuumiza usoni hivyo kuhukumiwa miezi kumi na mbili jela, huku adhabu halisi ikiwa ni miaka mitano.

Katika kesi hii Jaji alizingatia kuwa mtoto alikuwa na umri wa miaka 16, alikuwa kidato cha tatu na lilikuwa kosa la kwanza hivyo alimuachia huru akisema kuwa muda aliokuwa amekwisha kaa jela umetosha kama adhabu.

Kwa upande wa mama, Jaji alimuhukumu miezi mitatu badala ya kumi na mbili jela kwa sababu lilikuwa kosa lake la kwanza na hakuwa mkorofi kaika jamii.

Pia katika kesi hii Jji alisema vitu viwili vikuu vya kuzingatia, nanukuu;-
(i)           Pale ambapo mtuhumiwa amekutwa na hatia kwa mara ya kwanza basi mkazo uwekwe katika adhabu ya kumbadilisha, labda tu kosa liwe kubwa kiasi cha kuhitaji kutoa adhabu  ya fundisho au kosa liwe limeenea sana kiasi cha kuhitaji kutoa adhabu ya kuitisha jamii,

(ii)          Mtuhumiwa aliyekutwa na hatia kwa mara ya kwanza hapaswi kupelekwa gerezani ambapo anaweza kujichanganya na wahalifu sugu wa misimu ambao wanaweza mfundisha kuwa muhalifu.

Lakini pia katika Kesi ya Jamuhuri dhidi ya Kabula Mhoja[4] Mahakama kuu ilimuongezea adhabu ya mwaka mmoja jela, Kabula aliyehukumiwa na mahakama ya chini kifungo cha miaka minne
Katika kesi hii Kabula alivunja mikono ya mtoto wa miezi minne kwa kutumia mikono yake. Kabula hakubahatika kupata mtoto kutoka kwa mme wake ambaye alizaa nje ya ndoa na mwanamke mwingine. Hivyo kutokana na kejili za mme wake, kabula siku ya tukio alimtembelea mke mdogo wa mme wake nakuomba kumuona mtoto, alipokabidhiwa mtoto ndipo Kabula alivunja mikono ya mtoto huyo.

Kwa kuzingatia uzito wa kosa Mahakama kuu iliamua kubadilisha adhabu kutoka miaka minne hadi mitano wakati mtuhumiwa alikuwa ameomba apunguziwe adhabu.

Hivyo ni muhimu kutambua kuwa kuna kanuni ambazo mahakama lazima izingatie katika kutoa adhabu, na kanuni hizi zime ainishwa na sheria mbalimbali zinazotaja makosa hayo pamoja na kesi zilizokwisha amuliwa.



[1] The Minimum Sentence Act, Cap, 90, R.E. 2002
[2] R. V. Kidato Abdullah 1973 L.R.T. 82
[3] R. v . Asia Salum and Others 1986 T.L.R. 12
[4] R. v. Kabula Mhoja, 1986 T.L.R. 248

JINSI YA KUMLAZIMISHA SHAHIDI ALIYEKATAA KUJA MAHAKAMANI AJE MAHAKAMANI







Kumekua na dhana ya baadhi ya watu kuogopa Mahakama, hata pindi wanapoombwa kwenda kutoa ushahidi wa matukio walio shuhudia wao hukataa.

Sheria ya mwenendo wa madai [1] imetoa mwongozo wa kumlazimisha shahidi huyo kuja mahakamani kutoa ushahidi katika kesi yako.

Hivyo basi kupitia sheria hiyo utatakiwa kuiomba Mahakama kutoa wito wa shahidi kuhudhuria Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wowote ule unaotakiwa kutolewa kwa ajili ya kujenga kesi yako. Hivyo Mahakama itatoa wito wa shahidi kuhudhuria Mahakamani ( wengi huifahamu kwa jina samansi)

Endapo shahidi atakataa wito wa Mahakama, yani atagoma kuja mahakamani katika tarehe tajwa, Mahakama itatoa tangazo ambalo litabandikwa katika mlango wa nyumba anayoishi au sehemu yoyote ambapo mtu huyu anaweza kuliona tangazo hilo.

Mahakama pia inaweza kutoa amri ya kushikiliwa kwa mali ya shahidi huyo na dalali wa mahakama mpaka atakapo mlipa dalali wa mahakama pamoja na fine au mali zake kuuzwa vile Mahakama itakavyoona inafaa.

Njia nyingine ni kwamba Mahakama imepewa mamlaka yakutoa hati ya kukamatwa kwa shahidi huyo kwa dhamana au bila hata ya dhamana.

Hivyo basi unapaswa kutambua kuwa, pindi unapohitajika kwenda kutoa ushahidi Mahakamani, unapaswa kuitikia wito huo ili kuepukana na usumbufu kama ulivyo ainishwa katika sheria ya mwenendo wa madai


TRINITY COAST  ATTORNEYS,
POBOX 79490, 
DAR ES SALAAM,
5TH FLOOR DARWORTH (BAVARIA) HOUSE,
OFF NYERERE RD., KAMATA TRAFFIC LIGHTS
OPP. NAKUMAT SUPER MARKET






[1] (Chapter 33, order XVI rule 1 mpaka 10)




FAHAMU JINSI YA KUJENGA KESI YAKO KWA KUBOMOA USHAHIDI WA UPANDE WA PILI MAHAKAMANI

Makala hii inahusu watu wanaopeleka kesi zao mahakama ya mwanzo.
 Kwa Tanzania mahakama hii ndio mahakama isiyo ruhusu mawakili wasomi kuwakilisha wateja wao katika kesi mbali mbali ambazo zipo chini ya mamlaka ya mahakama hii.

Kutokana na hofu ya kuingia mahakamani, au kuhukumiwa watu wengi hushindwa kujitetea ipasavyo na mwisho kupoteza haki zao, hivyo basi hapa utajifunza jinsi ya kujenga kesi yako kwa kubomoa ushahidi wa upande wa pili.

Pindi unapopewa nafasi ya kumuuliza maswali shahidi, jaribu kwenda kwa mtiririko ufuatao.

Muulize shahidi maswali kama yeye anakufahamu, mahali unapoishi, wewe nay eye mlianzaje kufahamiana, shughuli zako unazo fanya, muulize kama anaufahamu mgogoro au kesi hiyo vilivyo, muulize pia kwanini yeye anasimama pale

Endapo unahisi shahidi huyu anatoa ushahidi kwa sababu ulishawahi kukosana nae hapo awali basi ijenge kesi yako kwa kumbana na maswali yanayo onyesha kuwa yupo hapo kwa sababu anakinyongo na wewe.

HUPASWI kuanza kumuuliza maswali yanayo husiana na siku ya tukio moja kwa moja, kwani unaweza kupoteza kesi yako hasa kama ni kesi ya kutengeneza yani watu wamepanga  waje wajenge mazingira ya wewe kufanya kosa hilo.

HIVYO mbane kadri uwezavyo kwa maswali kwa kujenga historia yake na wewe hapo awali kabla ya siku ya tukio au mgogoro. Ili kuweza kumsaidia mheshimiwa Hakimu kuwa Yule shahidi mmefahamianaje na kwa nini yeye ameingia kama shahidi dhidi yako


Unapopewa nafasi ya kuuliza maswali usimwambie hakimu kuwa “huyu ni muongo, siku hiyo mimi sikuwepo….” Mheshimiwa Hakimu hatokusikiliza kwani yeye amekupa nafasi ya kuhoji maswali na sio kujitetea.

Hivyo bomoa ushahidi na ijenge kesi yako kwa kumuhoji maswali shahidi tangu kabla mgogoro haujatokea mpaka ulipotokea ili hakimu aweze fahamu historia yenu na mpaka kupelekea mgogoro hapo Mheshimiwa hakimu atakukwa amepata story kamili kupitia maswali yako


TAMBUA kipengele hiki kimeongelea pindi mlalamikaji au mlalamikiwa anapopewa nafasi ya kubomoa ushahidi wa shahidi ni baada ya shahidi kutoa ushahidi wake wa awali kwa lugha ya kisheria tunaita CROSS EXAMINATION.

Vile vile ni vema kutembelea ofisi za mawakili kwa ajili ya ushahuri kabla ya kesi yako kusikilizwa. KUMBUKA Wakili Msomi hana majibu ya kesi yako ila pindi utakapo msimulia, atakuelekeza jinsi ya kuendesha kesi yako na si kukufundusha uongo.

Niimani yangu umejifunza japo kwa ufupi juu ya kubomoa ushahidi wa upande wa pili na hivyo ndivyo unavyoijenga kesi yako mbele ya Mahakama Tukufu.

Imeandaliwa na Mwanasheria Cuthbert

TAMBUA HAKI NA WAJIBU WAKO MBELE YA POLISI BARABARANI





Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati ganianakusimamisha uwapo barabarani.

Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako – kamaatakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani – pia anaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).

Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari – anaweza kukataa fotokopi – hata hivyo, unaweza kuamua kupeleka leseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa.Ili kuepukamatatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).

Hati ya usajili:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili – gari lazima liendane na maelezo yakwenye kibandiko, lakini vitu vidogokama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).

Leseni ya barabarani, na bima ya gari: 
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani nakibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).

Kunyang’anywa: 
Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.

Mikanda ya kiti ya usalama: 
Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) – unatendakosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.

Kuendesha baada ya kunywa pombe:​
Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi cha pombe kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatiaya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).

Kutumia simu ya mkononi wakatiunaendesha: 
ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la “​
kuendesha kwa uzembe” (RTA, s.42, s. 50).

Mwendo kasi: 
Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) – ofisa wa polisi anaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).

Kustahili kuwepo barabarani:
Ofisa WA polisi ana haki ya kukagua Kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri –unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.

KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA:
 Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwaofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezokwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini – kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda Na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIAYOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisianakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishi kwa Ofisa Msimamizi Mkuu – ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu –usitoe rushwa na usipokee rushwa. ​

SOURCE JAMII FORUM.

SHERIA ILIYOTUMIKA INAITWA THE ROAD TRAFIC ACT SURA YA 168.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BC LEGAL INFORMER - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger